Wednesday, August 3, 2011

MSANII ‘VITUKO SHOO’ ATAMBA KWA UKAHABA TANGA



Tunu katika pozi.
Na Dege Masoli, Tanga
MSANII Amina Mgonanze aka ‘Tunu’ ambaye ni miongoni mwa wasanii wanaotamba katika kipindi cha Vituko Shoo kinachorushwa na kituo cha telelvisheni Channel Ten, amekuwa gumzo katika Jiji la Tanga  kwa kuonyesha umahiri mkubwa wa kuigiza kama kahaba na hivyo kuwafanya kinamama wakazi wa........................
jiji hilo kuhofia waume zao kutekwa naye.

Msanii huyo  na wenzake kina Masele, Shalbal, Mzee Onyango, Majuto na Mwita wamepiga kambi katika jijini Tanga  chini ya kampuni ya  Al-Riyamy Production ya jijini Dar kwa ajili ya kuandaa kipindi hicho kinachorushwa na televisheni hiyo.

Hofu ya baadhi ya kinamama wa Tanga imetokana hasa na dhana kwamba kumudu kwa Tunu kuigiza kama kahaba, licha ya kuwa ni kivutio, kunaweza kuwafanya waume zao kumfuata kutokana na  kushawishika.

“Binti huyo ni kama kahaba kweli, na kama akiingia mitaani tumekwisha tutakuwa hatuna waume,” alieleza mmoja wa kinamama akimhofia msanii huyo.

Tunu  ambaye aliwahi  kucheza  kama katibu muhtasi wa Charles Magali ‘Mzee Magali’ akiwa na kikundi cha Watevu cha jijini Dar na kupata umaarufu mkubwa kabla ya kuhamia Al-Riyamy,  alionyesha umahiri  wa kuigiza kama  kahaba  wa  msanii maarufu nchini Masele aka Chapombe.

Katika sehemu hiyo Masele alionekana kama kijana mwenye pesa nyingi na anayezitumia kwa ajili ya mambo ya starehe ambapo Tunu na Tausi ndio mabinti anaofanya nao matanuzi, wakiigiza kama makahaba na wenye uwezo mkubwa wa kuwanasa wanaume wenye pesa.

Msanii huyo ambaye ni pacha na msanii  Tausi Mgonanze mbali na kuigiza na vikundi hivyo pia anaonekana sana katika kipindi cha Vituko Shoo cha Channel Ten akiigiza kama msichana aliyekumbana na mkasa wa kutapeliwa na mtu kutoka Mkongo.

HABARI KWA MSAADA WA GLOBAL PUBLISHER

No comments: